Kocha wa viungo Simba amuumbua Msenegal ,ataja sababu iliyomfanya ashindwe
Kocha wa viungo wa Simba, Mserbia, Dusan Momcilovic,
amefichua kuwa straika Msenegali, Papa Niang alidanganya kuwa yupo fiti wakati hakuwa fiti na hiyo ilichangia ashindwe katika majaribio ya kuichezea timu hiyo.
Momcilovic amesema baada ya Niang kutua klabuni hapo, alimuuliza kama yuko fiti ambapo mchezaji huyo alisema yupo fiti lakini haikuwa hivyo kwani hakuwa fiti.
“Niang alipokuja nilimuuliza kama yupo fiti akasema ndiyo na kudai siku tatu tu nyuma alitoka kucheza mechi na timu yake ya taifa, nilipompima nikagundua siyo kweli, hakuwa fiti, baadaye nikamuuliza kama anaweza kucheza, akasema ndiyo, alipopangwa ndiyo hivyo tena. Alihitaji zaidi ya siku 45 kuwa fiti kabisa,” alisema Momcilovic.
Aidha, taarifa nyingine zinadai straika huyo hakuwa amecheza kwa muda mrefu kabla ya kuja nchini, ndiyo maana katika mechi ya Mwadui FC alichemka.
Kocha wa viungo Simba amuumbua Msenegal ,ataja sababu iliyomfanya ashindwe
Reviewed by Steve
on
Friday, August 28, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment