Gareth Bale azungumzia uhusiano wake na Ronaldo klabuni Real Madrid, je ni kweli hawaelewani?
uhusiano wake na mchezaji mwenzie klabuni hapo, Cristiano Ronaldo.
Bale ameweka hali ilivyo kati yake na Ronaldo ambapo watu wengi walikua wakiamini kua wachezaji hao hazipikiki haziivi pamoja.
Tofauti na imani hiyo ya watu wengi, Bale amesema Ronaldo amekua kama muongozo wake klabuni hapo
"Kujifunza kutoka kwa mchezaji bora zaidi duniani ni kitu kikubwa sana" aliiambia WalesOnline.
"Ananikosha sana tangu niwasili hapa na nimekua najifunza vitu vipya kila siku.
"Ananisaidia sana mimi kuja kua mchezaji bora zaidi duniani, kitu ambacho ni lengo langu kubwa."
Pia Bale alisema anatarajia kufikia mafanikio ambayo Ronaldo anayo.
"Najitahidi kufikia level kama yake.
""Naangali mbele zaidi na kujua nini nitafanya" alimaliza Bale
Bale aliyejiunga Los Blancos mwaka 2013 akitokea Tottenham, amefunga magoli 39 na kutoa usaidizi mara 31 katika michezo 93 Santiago Bernabou.
Gareth Bale azungumzia uhusiano wake na Ronaldo klabuni Real Madrid, je ni kweli hawaelewani?
Reviewed by Steve
on
Friday, August 28, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, August 28, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment