Propellerads

Mesut Ozil ataja mchezaji anayeamini atafanya mabadiliko makubwa Man United



Nyota wa Arsenal, Mesut Ozil amemtaja mchezaji mmoja ambae
anaamini ataleta mabadiliko makubwa Man United msimu huu.

Kiungo huyo wa kati wa Arsenal anaamini Bastian Schwensteiger ndiye ataleta matumaini makubwa  kwa Man United msimu huu huku akiwashangaa wale wanaomponda mjerumani huyo mwenzie.

Lakini Ozil anaamini pia Schwensteiger atazima kelele za watu wanaomponda ndani ya kipindi kifupi kijacho.

"Vyombo vya habari vya Uingereza vinavyomkosoa havifanyi haki kwake" Ozil aliiambia tv moja ya kijerumani iitwayo Sport1.

"Bado anahitaji muda zaidi kuendana na Premier League, mpe muda kidogo tu.

"Basti ameuonesha ulimwengu mzima kwenye kombe la dunia kua kiongozi wa timu yukoje, mara nyingi katika fainali.

"Vyovyote vyombo vya habari vikiandika kuhusiana na Basti vinaanza na 'mshindi wa kombe la dunia'.

"Kwa sasa ni bingwa wa dunia ujerumani, ambaye ataleta makubwa Man United"

Schwensteiger amecheza mechi tano mpaka sasa na Red Devils ambapo ametoa usaidizi mara moja.


Mesut Ozil ataja mchezaji anayeamini atafanya mabadiliko makubwa Man United Mesut Ozil ataja mchezaji anayeamini atafanya mabadiliko makubwa Man United Reviewed by Steve on Friday, August 28, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.