Propellerads

Manchester United watangaza kumuuza beki wao kwa pauni mil 12



Klabu ya Manchester United wametangaza dau la
pauni mil 12 kwa klabu itakayomhitaji beki wake Jonny Evans.

Evans anaonekana kutokua na mchango wa kutosha kwa timu kipindi hiki kutokana na kuandamwa na majeraha na pia nidhamu mbovu uwanjani msimu uliopita.

Kocha Louis van Gaal hakupendezwa na tukio la kumtemea mate Papiss Cisse lililofanywa na nyota huyo ambapo ilimpelekea kufungiwa mechi sita.

Katika kipindi hiki cha usajili beki huyo amekua amehusishwa na vilabu vya West Bron na Everton lakini kwa bei hiyo ya Man United inaweza kua kubwa sana.

Evans amekua Old Trafford katika kipindi chote cha soka lake ambapo alianza kuonekana kwenye mechi dhidi ya Coventry katika League Cup, alichezea kwa mkopo vilabu vya Sunderland na  Royal Antwerp ya Uholanzi.

Akiwa Man united amecheza mechi 198 huku akichukua mataji matatu ya Premier League, moja la Club World Cup, mawili ya League Cup, na ngao ya hisani mara nne.
Manchester United watangaza kumuuza beki wao kwa pauni mil 12 Manchester United watangaza kumuuza beki wao kwa pauni mil 12 Reviewed by Steve on Wednesday, August 26, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.