Man United watenga ofa ya pauni 36.3m kwa mshambuliaji wa Monaco
Imeripotiwa kua Man United wametenga ofa ya
pauni mil 36.3 kwa ajili ya mshambuliaji wa AS Monaco, Anthony Martial.
Wakali hao wa Premier League wamekua wakidaiwa kua katika uhitaji wa kusajili mshambuliaji kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili hapo kesho.
Huku tayari wakiwa wamehusishwa na wakali kama Gareth Bale, Neymar na Thomas Muller, RMC Sport imeripoti kua Man United wako katika mazungumzo na Monaco juu ya Martial.
Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya U-21 ya Ufaransa, alisaini mkataba mpya na Monaco mwezi June na mpaka sasa ameshaifungia magoli 8 katika mechi 31 msimu uliopita.
Man United watenga ofa ya pauni 36.3m kwa mshambuliaji wa Monaco
Reviewed by Steve
on
Monday, August 31, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, August 31, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment