Tetesi za Usajili ulaya leo Jumanne.
Juve wamekanusha kupokea ofa ya Vidal kutoka Real Madrid
Juve wamekataa kua wamepokea
ofa yoyote kutoka kwa Real Madrid ili kumuuza nyota wake Arturo Vidal lakini wako tayari kumruhusu aondoke.
Barca kumsajili Turan
Inadaiwa kocha w Barca amezungumza na uongozi wa klabu ili kumnasa nyota wa Atletico Madrid, Arda Turan ambaye anajiandaa kuondoka Rojiblancos huku vilabu kama Chelsea, na Manchester Ubited vikionesha nia ya kumnasa.
Otamendi kutimka Valencia
Nyota Nicolas Otamendi anadaiwa kutaka kutimka kutoka klabu yake ya sasa ya La liga, valencia huku akitabiriwa kwa kiasi kikubwa kutua Manchester United.
Arsenal bado wanamwinda pedro
Arsenal bado wako katika mbio za kumtoa Pedro Barcelona na kumleta London. Japo nyota huyo ameongeza mkataba wake wa sasa na Barcelona, lakini klabu bado iko tayari kwa mazungumzo ya kumuuza. Vilevile Arsene Wenger anadaiwa kufanya mazungumzo na wakala wa Pedro.
Liverpool kumsainisha Benteke
Liverpool wako kwenye mchakato wa kupata wakali wapya, miongoni mwao ni nyota wa Aston villa
Christian Benteke ambaye wakikamilisha usajili wake atawagharimu kiasi cha pauni mil. 32.5
Kwingineko wakali wa soka Uturuki , Fenerbahce wametangaza kumsainisha nyota wa zamani wa Man united Louis Nani kwa dau la pauni mil 6 mkataba wa miaka maitatu, Tottenham wamemuuza kiungo wao Etiene Capoue kwa timu iliyopanda daraja msimu huu Watford kwa dau la pauni mil. 7, huku Valencia wakimsajili nyota wa PSC Zakaria Bakalli kwa uhamisho huru.
Tetesi za Usajili ulaya leo Jumanne.
Reviewed by Steve
on
Tuesday, July 07, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Tuesday, July 07, 2015
Rating:



