Propellerads

Ngoma afunguka ya moyoni Yanga.



Nyota mpya aliyesajiliwa na Yanga msimu huu akitokea FC Platinum ya Zimbabwe Donald Ngoma, amefunguka
ya moyoni tangu ajiunge klabuni hapo.
“Nina furaha kujiunga na Yanga, ni miongoni mwa klabu kubwa Afrika ina uongozi bora, mashabiki bora, waalimu bora pia na kikosi bora. Hatukutegemea (yeye na Zuttah) kama tungepata mapokezi kama haya kutoka kwa mashabiki tumeshangazwa sana na jinsi mashabiki walivyo wengi na wanavyoipenda timu yao”, amesema Ngoma
Najua kuchezea klabu kubwa kama hii kuna presha kubwa sana lakini naamini nitaishinda hiyo presha na kufanya kile mashabiki wanachotarajia kutoka kwangu, siwezi ahidi chochote zaidi ya kusema kazi yangu uwanjani ndio itatoa majibu”, alisema Mzimbabwe huyo.

SOMA: KERRY ATOA ONYO KWA WAVIVU
Donald Ngoma Dombo anaondoka leo kurudi kwao kwa ajili ya kujiandaa rasmi ili kuja kuitumikia Yanga ambapo atarudi Jumapili na siku ya Jumatatu ataanza mazoezi kujiandaa na michuano ya Kagame.
Ngoma afunguka ya moyoni Yanga. Ngoma afunguka ya moyoni Yanga. Reviewed by Steve on Thursday, July 02, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.