Propellerads

Drogba ataja mabeki waliokua mwiba kwake.




Mkongwe wa Chelsea, Didier Drogba, ametaja  mabeki ambao alihangaika haswa pindi alipokutana nao wakati
alipofanya interview na Rio Ferdinand.

Mkali huyo alimwambia Ferdinand kua alikua miongoni mwa mabeki wagumu aliopata kukutana nao, pia na aliyekua mchezaji mwenzie Man U, Nemanja Vidic pamoja na aliyekua beki wa FC Barcelona, Carles Puyol.

"Kila wakati hua ninasema ni wewe na Vidic" alimwambia Rio Ferdinand ambaye yupo BT Sports kwa sasa.

"Naweza kusema kila nilipofunga dhidi ya Man United ilikua kweli, nilikua na furaha kwa sababu sikuweza kuwafunga sana"

"Kwa hiyo mimi kuwafunga  nyie naweza kusema nilikua na mchezo mzuri"

"Ni  nyinyi wawili na Carles Puyol"

"Kwa sababu ana nguvu na ni mlinzi mzuri, lakini ni gentleman"

Drogba ameweza kuifungia Chelsea magoli 164 katika mechi 381 huku akitoa usaidizi mara 88
Drogba ataja mabeki waliokua mwiba kwake. Drogba ataja mabeki waliokua mwiba kwake. Reviewed by Steve on Tuesday, July 07, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.