Propellerads

Wakala wa Raheem Sterling afunguka kiivi

Wakala wa Raheem Sterling, Aidy Ward amedai habari za mshambuliaji huyo kuondoka Liverpool majira ya kiangazi mwaka huu zimekuzwa kwa kiasi kikubwa na
vyombo vya habari.

Sterling


Ward ambaye ni wakala wa muda mrefu wa Sterling amesema yeye pamoja na mchezaji wana ratiba ya kukutana na maafisa wa Liverpool juma hili na kuanzia hapo wataweka wazi kila kitu.
Sterling amebakiza miaka miwili katika mkataba wake wa sasa, lakini amekataa mshahara wa paundi laki moja kwa juma ulioripotiwa mapema mwaka huu na mazungumzo juu ya mkataba mpya yakasitishwa mpaka mwishoni mwa msimu huu.
Mwezi uliopita imeelezwa kuwa Sterling hana nia ya kusaini mkataba mpya na anasubiri ofa za majira ya kiangazi, huku kocha wa Arsenal,  Arsene Wenger akishindwa kukanusha taarifa za kuitaka saini ya nyota huyo wa Liverpool.
Wakala wa Raheem Sterling afunguka kiivi Wakala wa Raheem Sterling afunguka kiivi Reviewed by Steve on Tuesday, May 19, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.