Kama De Gea ataondoka, huyu anapigiwa debe kumrithi.
Victor Valdes ameungwa mkono kuwa mlinda mlango chaguo la kwanza wa Manchester United kama David De Gea ataondoka
Old Trafford majira ya kiangazi mwaka huu.
De Gea ambaye mkataba wake unamalizika 2016 anahusishwa kujiunga na Real Madrid , huku kocha wa Manchester United, Louis van Gaal akikiri ugumu wa kumzuia kipa huyo wa zamani wa Atletico kurudi nyumbani kwao.
![]() |
| De Gea(kushoto) na Valdes |
Van Gaal tayari anajua nani atamrithi De Gea kama anaondoka, lakini vyombo vya Hispania vinapendekeza kwamba Mholanzi huyo aliyefanya kazi na Valdes akiwa Barcelona, hivyo anaweza kuvutiwa kumchagua kuwa kipa chaguo la kwanza.
Kipa wa zamani wa Man United, Raimond van der Gouw amesema kuwa Valdes anaweza kuwa chaguo sahihi kumrithi De Gea kwasababu ya uzoefu wake na aina ya udakaji wake .
Edwin van der Sar aliichezea United mpaka alipofikisha miaka 40, alistaafu 2011 baada ya kuisaidia timu kubeba makombe manne ya ligi kuu na ligi ya mabingwa mwaka 2008 na Van der Gouw amesema Van der Sar alifanya kazi kubwa licha ya umri kwenda.
Wakati akipigiwa chapuo hilo, Valdes ambaye alicheza mechi yake ya kwanza katika sare ya 1-1 dhidi ya Arsenal amesema hajui kitakachotokea msimu ujao, lakini ana furaha ya kukaa Old Trafford.
Kama De Gea ataondoka, huyu anapigiwa debe kumrithi.
Reviewed by Steve
on
Wednesday, May 20, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, May 20, 2015
Rating:



