Propellerads

Tetesi: Guardiola kuitema Bayern, kujiunga Man City

Meneja wa Bayern Pep Guardiola ameripotiwa kutaka kuondoka klabuni hapo ili akajiunge matajiri wa kiarabu Man City, kama ripoti ni za kuaminika.

Mhispania huyo alipata mafanikio makubwa alipokua Barcelona na Bayern pia ambapo mpaka sasa anashikilia taji la Bundesliga kwa mara ya pili mfululizo. Hata hivyo kulingana na jarida la beIN Sport Middle East, kushindwa kwa Bayern 3-0 dhidi ya Barcelona UEFA kumemletea presha katika kibarua chake.

                                            
                                                
Guardiola
                                     

Pia Manuel Pellegrini nae anahaha kuhusu kibarua chake inaelekea makocha hawa wakapishana majira ya kiangazi. Kushindwa kwa Guardiola kuleta ndoo ya UEFA Bayern kumepelekea kuwepo ukosolewaji mwingi, lakini kwa kiwango chake inatosha kabisa kumshawishi tajiri wa Man City kua anaweza kuipa nguvu tena klabu yake.

Kwa kuongezea tetesi zinasema kua jinsi Guardiola alivyo na mgogoro na madaktari wa timu, pia vitendo vyake vya kushangaza siku za hivi karibuni inaashiria kabisa uhusiano wake na klabu unapumulia mashine.

Pep Guardiola ameshinda mataji 18 ndani ya misimu saba ya safari yake ya ukocha, mawili yakiwa ni ya UEFA
Tetesi: Guardiola kuitema Bayern, kujiunga Man City Tetesi: Guardiola kuitema Bayern, kujiunga Man City Reviewed by Steve on Monday, May 11, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.