Propellerads

Mambo matano usiyoyafahamu kuhusu mchezaji mpya wa man u, Memphis Depay

Mholanzi huyu ametawala Headlines za vyombo mbali mbali baada ya kusaini mkataba wenye thamani ya pauni mil 30 na mashetani wekundu, pia katika kufananishwa kwake na Christiano Ronaldo.
Msomaji yawezekana kabisa una shauku ya kutaka kumfahamu kwa undani zaidi mholanzi huyu, leo nakuletea mambo matano ambayo unaweza
ukawa huyafahamu kuhusu Depay




                   
Depay
                                      
1)Ni mchezaji mdogo kabisa kuwahi kuifungia Uholanzi kombe la dunia.

Akiwa na miaka 20 tu alifanikiwa kua mchezaji mwenye umri mdogo kabisa kuwahi kuifungia uholanzi kwenye michuano ya kombe la dunia, hii ilikua mechi dhidi ya Australia katika hatua za makundi.

2)Ana damu ya ki-afrika

Memphis Depay alizaliwa 1994 huko kusini mwa uholanzi mji wa Moordrecht, baba mghana huku mama akiwa ni mholanzi.

3)Kwenye jezi ameandika jina la 'Memphis' pekee

Alipokua na umri wa miaka minne tu wazazi wake waliachana hivyo alilelewa na mama yake na wazee upande wa mama. Amekua na machungu ya kutelekezwa na baba labda ndo sababu hapendi kutumia jina la Depay ambalo ndio jina la baba yake mzazi, pia baba yake hana mawasiliano na familia.

4)Ni mpenzi mkubwa wa tattoos

Depay ana tatoo nyingi mwilini mwake na mojawapo kajichora kama kumbukumbu kwa baba yake ambaye alifariki siku Depay anatimiza miaka 15. Baba yake alikua ni kama baba pia kwake na alihudhuria michezo yote Depay aliyocheza mpaka umauti ulipomfika.

5)Anafananishwa na Cristiano Ronaldo


Mchezaji wa zamani wa Man u ,Scout amemfananisha ujio wake kama Ronaldo mwingine tena Man u
"Ana ujuzi kama ulu ule wa Ronaldo alipokua kinda. Ana mbinu hatari, mjuzi, yuko chap, ana rekodi nzuri ya ufungaji, anaweza kupiga shuti umbali wowote-ana kila kitu" alisema scout



Mambo matano usiyoyafahamu kuhusu mchezaji mpya wa man u, Memphis Depay Mambo matano usiyoyafahamu kuhusu mchezaji mpya wa man u, Memphis Depay Reviewed by Steve on Monday, May 11, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.