Propellerads

Neymar "Nazidi kumpenda Messi kila siku"

Fowadi wa FC Barcelona Neymar amesema kua anazidi kumpenda Messi zaidi kila siku, kwa madai kua Messi si mbinafsi ndani na nje ya uwanja.

                                   
Messi akiwa na Neymar

Messi na Neymar walishirikiana vyema katika
kuitungua Bayern Munich 3-0 jumatano iliyopita katika mechi ya UEFA.

Akiongelea ubora wa Messi, Neymar mechi dhidi ya Cordoba ambapo walishinda 8-0, amesifia jinsi Messi alionesha hakua na tamaa ya kupata hat trick baada ya kumpa Neymar apige penati ambayo kama messi angepiga angepata ha trick.
 "kilikua ni kitu kidogo nafikiri, lakini lilikua ni jambo jema" alisema Neymar
 "Ni mtu ambaye ni bora duniani, ilikua afunge apate hat trick lakini akaniachia nipige penati ile
  "Nilishikwa na butwaa, namshukuru sana kwa ukarimu, kila siku najifunza kutoka kwake. Anaitendea vyema historia ya soka, nampenda Messi, namkubali zaidi kila siku zinavyokwenda"

Neymar amecheza mechi 45 Barca akifunga magoli 34 ametoa usaidizi mara 1o
Neymar "Nazidi kumpenda Messi kila siku" Neymar "Nazidi kumpenda Messi kila siku" Reviewed by Steve on Sunday, May 10, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.