Propellerads

Ronaldo ajaye Man u ni zaidi ya CR 7 kwa umri wake?

Manchester United wamemsainisha Memphis Depay kwa dau la pauni milioni 30 akitokea, Hata hivyo ujio wa mchezaji huyu Man u wamefanaisha na ujio wa Ronaldo kipindi kile, hivyo ni kama Ronaldo 'anayefatia' tena Man u, lakini inakuaje mholanzi huyu afananishwe na Ronaldo wa kipindi kile akiwa na miaka 21?
 Wengine wameenda mbali zaidi na kuamini kua Depay ni
bora zaidi kuliko Ronaldo kipindi kile

                                                 
Ronaldo alipokua Man u

De pay

Tofauti na Ronaldo, Depay anaingia EPL akiwa tayari ana jina kubwa tu huko ligi ya kwao Uholanzi-Dutch Eredirisie ,wakati Ronaldo aling'aa na kupata jina akiwa tayari amejiunga Old Trafford na kufanikiwa kuchukua Ballon d'or yake ya kwanza 2008 chini ya Sir Alex Ferguson,

Pia ukifatilia takwimu za soka ukianzia Ureno mpaka kufikia msimu wa 2005/06 Ronaldo alipokua na umri sawa na Depay wa miaka 21 Ronaldo hakua na rekodi yoyote kubwa, wakati Depay tayari anazo.

Ronaldo alicheza mechi 131 katika misimu mitatu ya mwanzo Old traford akifunga magoli 26 katika michuano yote, wakati Depay amecheza michezo 122 katika timu yake ya kwanza na kufunga magoli 49.

Ronaldo alifanikiwa kuchukua mataji mawili, FA 2003/04 na ubingwa wa ligi 2005/06 akiwa na Man u, wakati Depay ana mataji matatu kwa kipindi mpaka kufikia sasa ambayo ni, KNVB cup 2011/12 na Johan Cruff 2012

Wote wamefunga magoli kila mmoja katika mechi zao za mwanzo kimataifa , Ronaldo akiwa na miaka 19 kombe la Euro 2004 na Depay akiwa na miaka 20 kombe la dunia 2014.

Cha kushangaza zaidi wote wamezaliwa februari!!

Wakati wa kuyathibitisha haya tunaungoja sas!!
Ronaldo ajaye Man u ni zaidi ya CR 7 kwa umri wake? Ronaldo ajaye Man u ni zaidi ya CR 7 kwa umri wake? Reviewed by Steve on Sunday, May 10, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.