Propellerads

Ronaldo: Mpira hauna nyota wa kutosha.

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil na Real madrid Ronaldo De Lima , amedai ukiwatoa Messi na Ronaldobado soka halijapata nyota wa kutosha.

Akikubaliana na kauli ya mchezaji mwenzie wa zamani pale Real Madrid, Zinedine Zidane aliyesema Messi, Neymar na Ronaldo ni wachezaji wakubwa lakini soka bado
halijapata nyota wa kutosha.
               
                                                   

"Kama alivyosema Zidane, nadhani Messi ni mkali, Ronaldo pia, na Neymar lakini naona soka bado limekosa nyota wa kutosha" aliiambia Marca.

Hata hivyo pamoja na kukubaliana na kauli ya Zidane, Ronaldo amedai kua hafikirii kua kocha siku moja kwa sababu anawaza jinsi alivyokua akipata presha uwanjani kama mchezaji tuu sasa itakuaje akiwa kama kocha!!

Ronaldo katika professional career yake amecheza mechi 423 akifunga magoli 277 na kutoa usaidizi mara 64.
Ronaldo: Mpira hauna nyota wa kutosha. Ronaldo: Mpira hauna nyota wa kutosha. Reviewed by Steve on Tuesday, May 12, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.