Propellerads

Maradona: Magolikipa wanamwogopa zaidi CR7 kuliko Messi

Mkongwe wa soka muarjentina Diego Maradona amedai makipa wengi wanamwogopa Ronaldo kuliko Messi.

Alisema wachezaji wote- Ronaldo na Messi wapo katika viwango sawa kwa sasa ukijaribu kuwafananisha, lakini akaongezea
CR7 ndio anaogopeka zaidi na makipa wengi.

               



"Sio swala kwamba Messi ni zaidi ya Ronaldo au Ronaldo ni zaidi ya Messi" Aliiambia Sky sports.

"Nadhani wako katika kiwango sawa .

"Cristiano ni mnyama mbele ya goli, huwezi kumuachia akapiga shuti kutokea nusu ya uwanja kuelekea kwa wapinzani.

"Magoli kipa wanamwogopa, inabidi uwe mkweli makipa wanamwogopa.

"Hawamwogopi Messi kwa sababu hana nguvu kama ya Ronaldo.

"Cristiano ni fundi, Nafikiri kwa hiki kipindi anastahili kabisa kuwepo kiwango cha Messi.

Msimu huu Ronaldo ana magoli 54 kati ya michezo 51, wakati akitoa usaidizi mara 21

Messi amefunga 53 kati ya mechi 52, akitoa usaidizi mara 30.


Maradona: Magolikipa wanamwogopa zaidi CR7 kuliko Messi Maradona: Magolikipa wanamwogopa zaidi CR7 kuliko Messi Reviewed by Steve on Tuesday, May 12, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.