Propellerads

Mourinho kafichua siri ya kumdhibiti Messi

Bosi wa Chelsea Jose Mourinho ametoa mbinu ambazo kocha yeyote anaweza kutumia kumdhibiti mshamuliaji hatari wa FC Barcelona Lionel Messi.

Kocha huyo amepata kukumbana na Messi mara kibao wakati alipokua
akiinoa Real Madrid, pia katika nusu fainali ya UEFA 2010 alipokua Inter vile vile akiwa kama meneja wa Chelsea.

                                               

Mourinho amefichua siri kua alitumia muda mwingi kujipanga namna ya kumdhibiti Messi, ambapo anadai hicho pekee na juhudi ya timu ndo dawa ya Messi, na si vinginevyo!!

"Nilijipanga kila nilipokutana nae. Nilitumia muda mwingi kumsoma na kutafuta mbinu za kupambana nae." Alisema Mourinho kama alivyoripotiwa na jarida la squawka.

"Mara nyingi tulifanikiwa, muda mwingine tulishindwa. Inter dhidi ya Barcelona tulimdhibiti mechi zote. Nimekumbana nae mara kadha wa kadha."

"Kila nilipokutana nae nilifikiria ni mbinu gani ambayo tungetumia kumdhibiti, hicho ndio kikubwa kumdhibiti Messi"

Messi amefunga magoli 11 kati ya mechi 24 alipocheza na timu zilizokua chini ya Mourinho, huku akashindwa kufunga mara 16.
Mourinho kafichua siri ya kumdhibiti Messi Mourinho kafichua siri ya kumdhibiti Messi Reviewed by Steve on Tuesday, May 12, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.