Propellerads

Mapunda:Naamini nimefanya kazi nzuri.

Kipa mkongwe wa Simba Ivo Mapunda amesema anamatumaini ya kuendelea kuichezea timu hiyo msimu ujao licha ya kutokuwepo na dalili zozote za mazungumzo na viongozi wa timu hiyo inayopigania kumaliza nafasi ya pili msimu huu.


                                                 


Ivo Mapunda mwenye mchango mkubwa kwenye kikosi cha Simba tangu atue kwenye mzunguko wa pili msimu uliopita akitokea Gor Mahia ya Kenya ameiambia Kandanda angependa kuendelea kuichezea timu hiyo kutokana na kazi nzuri aliyoifanya lakini ameuachia uongozi na benchi la ufundi ili kuamua.
“Naamini nimefanya kazi nzuri katika msimu mmoja na nusu niliofanya kazi hapa Simba lakini kama mchezaji siwezi kulazimisha nimewaachia viongozi na benchi la ufundi kama wataona nafaa watanifata tuzungumze nadhani hatutoshindwa kwa sababu tumefanya kazi kwa pamoja na tunajuana,”amesema Mapunda.
Mkataba wa Mapunda mwenye umri wa miaka 31, unamalizika Mei 20/ 2015, na kiwango chake kimekuwa msaada kwa Simba licha ya makosa machache yaliyoigharimu timu yake msimu huu na kusababisha kupoteza baadhi ya mechi ikiwemo ile ya Kagera Sugar iliyochezwa uwanja wa taifa Dar es Salaam ambapo alimtemea Atupele Green mpira uliorushwa na Salum Kanoni na kumweka katika utata.
Mapunda:Naamini nimefanya kazi nzuri. Mapunda:Naamini nimefanya kazi nzuri. Reviewed by Steve on Monday, May 11, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.