Fabregas kuvunja rekodi ya Thiery Henry??
Midfielder wa Chelsea, Cesc Fabregas amebakisha mechi mbili ili avunje rekodi iliyowekwa na aliyekua mchezaji mwenzie Arsenal, Thiery Henry.
Forward wa zamani pale The Gunners, Henry anashikilia rekodi ya kutoa usaidizi mara nyingi zaidi katika ligi kuu ya Uingereza, Ambapo Fabregas ameongelea kuikaribia rekodi ya Henry ameshatoa usaidizi mara 18 mpaka sasa , huku rekodi iliyopo ni usaidizi mara 20 iliyowekwa na Henry.
![]() |
| Fabregas na Henry |
"Sasa tumekua mabingwa nitakua nadanganya kama nitasema hilo halikunitia msisimko" Aliiambia El partido de las 12.
"Jana nilimwambia Eden Hazard Nitakupasia mpira, na wewe utapiga mashuti kila saa.
"Kwanza, Nina furaha kuvunja rekodi yangu binafsi ya mara 17"
Henry aliweka rekodi hiyo msimu wa 2002/03, Fabregas anatarajiwa kuivunja rekodi hiyo kwa michezo miwili ya Chelsea iliyo bakia.
Fabregas kuvunja rekodi ya Thiery Henry??
Reviewed by Steve
on
Monday, May 18, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, May 18, 2015
Rating:



