Propellerads

Mourinho naye azungumzia kiwango cha Rooney, atoa ukweli wake




Bosi wa Manchester United, Jose Mourinho amemkingia
kifua nahodha wa kikosi chake anayepondwa, Wayne Rooney.

Uwezo wa mshambuliaji huyo umekua ukitia shaka siku za hivi karibuni huku akikosolewa na wadau mbali mbali wa soka.

Hata hivyo Mourinho amesisitiza kwamba matatizo ya timu yake ambayo yamekuja baada ya vipigo viwili mfululizo Premier League ni makubwa zaidi ya kiwango cha Rooney kinavyosuasua.

"Sisi ni timu. Sisi sio Rooney. Tulianza vizuri, tulishinda mechi nne, na tulipoteza mechi tatu ndani ya wiki, kwa hiyo haiwezi kua Wayne Rooney," Mourinho aliwaambia waandishi.

"Kusema ukweli hakucheza dhidi ya Feyernood, kwa hiyo ana mchango moja kwa moja mechi mbil. Tulikua na mwanzo mzuri wa msimu, bora kuliko hata tulivyojiandaa na kutarajia, na tulikua na hatia ya kukata matumaini ya watu kupoteza mechi tatu mfululizo."
Mourinho naye azungumzia kiwango cha Rooney, atoa ukweli wake Mourinho naye azungumzia kiwango cha Rooney, atoa ukweli wake Reviewed by Steve on Friday, September 23, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.