Propellerads

Gareth Bale anataka kuondoka Real Madrid, kisa hawa wawili




Gareth Bale ameripotiwa kua ameweka wazi kwamba anataka
kuondoka Real Madrid baada ya kutokua na furaha na rais Florentino Perez na meneja Zinedine Zidane.

Nyota huyo alihamia Bernabeu kwa ada iliyoweka rekodi ya dunia kwa wakati huo ya pauni mil 86 mwaka 2013 ambapo ameshaifungia Real Madrid magoli 49 katika mechi 85 za La Liga.

Kwa mujibu chapisho kutoka Hispania, Diario Gol, mshambuliaji huyo amekua akikosa furaha klabuni hapo tangu mwaka jana na sasa anaangalia namna ya kuondoka klabuni hapo.

Imedaiwa kua Perez alimuahidi Bale mkataba mpya pamoja na kumwongezea mshahara mwaka jana lakini mpango huo haujafanyika, huku raia huyo wa Wales akitajwa kuishi chini ya kivuli cha Ronaldo ambaye anaamini anapata upendeleo zaidi kutoka kwa Zidane.

Bale alitolewa na kuingizwa Lucas Vazquez katika dakika ya 70 Madrid walipopata sare ya 1-1 nyumbani dhidi ya Villareal Jumatano, maamuzi ambayo yalimkasirisha.

"Aliondoka uwanjani amekasirika," chanzo kililiambia chapisho hilo "Hakuelewa kutolewa kwake. Alihisi anastahili kucheza zaidi kuliko Cristiano Ronaldo na [Karim] Benzema. Lakini kwa mara nyingine tena alikuwa wa kutolewa."


Gareth Bale anataka kuondoka Real Madrid, kisa hawa wawili Gareth Bale anataka kuondoka Real Madrid, kisa hawa wawili Reviewed by Steve on Sunday, September 25, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.