Wenger asisitiza kua wana matarajio makubwa ya kushinda UEFA
Arsene Wenger amedai kua timu yake ina hamasa kubwa ya
kushinda michuano ya UEFA msimu huu.
The Gunners wataumana na Dinamo Zagreb usiku wa leo huko Croatia na wana matazamio ya kuanza michuano hiyo kwa ushindi ili kupata point tatu muhimu.
Katika fainali tano zilizopita Arsenal wamekua wakiishia katika mzunguko wa 16 pekee ambapo mafanikio makubwa pekee ni pale mwaka 2006 walipofikia fainali ambapo walipoteza mbele ya Barcelona.
Sasa Wenger anaamini wako katika nafasi nzuri tangu walipotolewa kwenye michuano hiyo na Monaco mwaka jana.
"Tulipoteza mchezo mmoja msimu uliopita, ulikua ni nyumbani dhidi ya Monaco" Wenger aliiambia Arsenal Player "Hatukua vizuri kiasi cha kutosha na tulitaka kuonesha tofauti katika mcheo wa kwanza.
"Tunajua kuna kitu cha kuangalia, ni kujuta tulivyopoteza mwaka jana. Kwa hiyo tutaonesha kile tulichojifunza kwa mwaka jana.
"Hii hamasa (ya kushinda) ni kubwa. Haijawai kua kwa Arsenal.
"Kwa upande mwingine nimekua kazini kwa muda mrefu kujua ukweli na wapi pa kujituma."
Wenger asisitiza kua wana matarajio makubwa ya kushinda UEFA
Reviewed by Steve
on
Wednesday, September 16, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, September 16, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment