Propellerads

Rio Ferdinand alivyomnanga Van Gaal kwa kuharibu mfumo wa Man United



RIO FERDINAND amemtupia lawama kocha Louis van Gaal kwa
kuharibu aina nzuri ya uchezaji iliyokua nayo Manchester United.

Red Devils kwa miaka iliyopita walisifika kwa kua na mpira wenye kasi ya ushambuliaji ambao kwa kiasi kikubwa ulijengwa na sir Alex Ferguson.

Hata hivyo ujio wa kocha Van Gaal umeleta mabadiliko makubwa Old Trafford ambapo Ferdinand anaamini hayana ubora wowote

Ameiambia  London Evening Standard kua "Nini tofauti ya falsafa Manchester United chini ya Van Gaal na chini ya Ferguson? kila kitu ni tofauti.

"Ukisema wachezaji, wako tofauti kabisa, na jinsi wanavyocheza. Ukiifananisha Manchester Unied yenye nguvu, ushambuliaji, lakini kwa sasa haiko hivyo.

"Mashabiki wa Man United wanatakiwa waelewe wenyewe kwa ambacho wataenda kushuhudia. Huwezi kushuhudia kile tulichokiona miaka 25 iliyopita.

"Itakua ni aina tofauti kabisa ya mpira, sio mpira niliofurahia kuona vile vile hata mashabiki wengi wa Man United.

Ungana nasi kupitia Facebook kwa ku like ukurasa wetu wa Kandanda 24 na tuffollow Twitter @Kandanda 24


Rio Ferdinand alivyomnanga Van Gaal kwa kuharibu mfumo wa Man United Rio Ferdinand alivyomnanga Van Gaal kwa kuharibu mfumo wa Man United Reviewed by Steve on Friday, September 11, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.