Propellerads

Kuelekea usajili januari: Mourinho amtaka nyota wa Man United,




Katika kuelekea kwa usajili mwingine Ulaya mwezi januari,
imeripotiwa kua Arsenal na Chelsea wako katika kinyang'anyiro cha kumnasa kiungo wa klabu ya Anderlecht, Youri Tielemans.

Hii ni kwa mujibu wa Calciomercato ambao wanadai kua klabu hiyo ya Ubelgiji inataka kiasi cha pauni mil 14.4million kwa ajili ya kinda huyo mwenye miaka 18.


Kwingineko, mkongwe wa Liverpool Steven Gerard amefichua kua alijaribu kumshawishi Willian ajiunge na Liverpool kabla ya Mbrazili huyo hajaamua kuelekea Stamford Bridge kwa pauni mil 32.

Katika kitabu chake cha 'My Story' amesema kua alijaribu kushwishi wengi wakubwa kuja Liverpool , mwaka 2013 mchezaji wa mwisho alikua Willian.

Mwisho kabisa kocha Jose Mourinho amedaiwa kua katika mpango wa kumnasa mlinda mlango wa Man United Victor Valdes katika dirisha la usajili mwezi januari.

Mchezaji huyo alijiunga na Man United yapata miezi nane iliyopita lakini amejikuta akiangukia chaguo la tatu tangu kuwasili kwa Sergio Romero msimu huu.

Ungana nasi kupitia Facebook kwa ku like ukurasa wetu wa Kandanda 24 na tuffollow Twitter @Kandanda 24
Kuelekea usajili januari: Mourinho amtaka nyota wa Man United, Kuelekea usajili januari: Mourinho amtaka nyota wa Man United, Reviewed by Steve on Monday, September 14, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.