Propellerads

Yanga ikifanya yake...taswira nzima na picha hapa!!



Yanga imefanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya Kagame ikitokea Kundi A ikiwa ni baada
ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KMKM.



Katika mechi hiyo yenye kasi kubwa, Yanga ilipata ushindi huo kupitia kwa bao la Malimi Busungu.



Kabla ya beki wa KMKM kujichanganya na Amissi Tambwe kuupiga mpira uliompita kipa Nassor Abdullah na kuandika bao la pili.



Mpira ulikuwa wa kasi na ushindani mkubwa huku KMKM wakitoa upinzani mkali ingawa katika dakika 30 za mwisho, walionekana kulishinda ‘rigwaride la Yanga’.



Yanga sasa imefikisha pointi sita baada ya mechi tatu, ikiwa imepoteza moja dhidi ya Gor Mahia.

Ita,alizia meechi ya mwisho dhidi ya Al Khartoum yenye pointi saba, Jumapili. Iwapo itashinda itakuwa imefikisha pointi 9 na kuwa katika nafasi ya pili au ya kwanza ingawa itasubiri pia matokeo ya Gor Mahia na Telecom.




Katika mechi ya kwanza, Gor Mahia ilitoka sare ya mabao 1-1 dhidi ya Al Kharthoum.


Yanga ikifanya yake...taswira nzima na picha hapa!! Yanga ikifanya yake...taswira nzima na picha hapa!! Reviewed by Steve on Friday, July 24, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.