Propellerads

Arsenal kumnasa Lewandowski!?




Arsenal wameripotiwa kutaka kumuwinda mshambuliaji nyota wa Bayern Munich
Robert Lewandowski kama tu dili la kumpata Karim Benzema litashindikana.

Karim benzema amekua akihusishwa sana na kutaka kuhamia Arsenal ambapo kocha Arsene Wenger anataka kuimarisha safu ya ushambuliaji kwa ajili ya msimu unaotarajiwa kuanza.

Imeelezwa kua Benzema ana uelekeo mkubwa wa kuelekea kwa wakali hao wa kaskazini mwa London ingawa wakala wake amesema kua uhamisho huo sio wa kutumainiwa sana.

Kwa sababu hii Arsenal wanafikiria kumfukuzia Lewandowski ambaye alihamia Bayern akitokea kwa mahasimu wao wakubwa Borussia Dortmund mwaka jana.

Kwa mujibu wa El Confidencial , The gunners wanataka kumuweka kwenye target mkali huyo anayetokea Poland kama mbadala wa Karim Benzema itakaposhindikana kumpata.

Hata hivyo Man United nao tayari walisharipotiwa kumuwinda lewandowski ambapo tayari wameshamnasa nyota mwingine wa Bayern, Schwensteiger.

Lewandowski amefunga magoli 24 katika mechi 47 alizoichezea Bayern.
Arsenal kumnasa Lewandowski!? Arsenal kumnasa Lewandowski!? Reviewed by Steve on Friday, July 24, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.