Propellerads

Mishahara ya nyota wapya waliosajiliwa Man United hii hapa.




Manchester United tayari wamewasajili wakali Bastian Schwensteiger, Memphis Depay, Matteo Darmian na Morgan Schneiderlin, vyombo vya
vya habari Uingereza vimeanika mishahara wanayovuta nyota hao.

Kwa mujibu wa Telegraph Man United wamepunguza mzigo wa Pauni mil. 30 za mishahara kwa kuwaruhusu Radamel Falcao, Nani na Van Persie kuondoka.

Ripoti zinaeleza zaidi kua mishahara ya nyota hao wapya imepungua kidogo kuliko ya wale walioondoka klabuni msimu huu.

Falcao alidaiwa kujikusanyia kiasi cha pauni mil 13.7 kwa mwaka aliokaa klabuni hapo, ambapo alilipwa pauni 265 000 kwa wiki.

Van Persie pia alikua ni miongoni mwa nyota wenye mishahara mikubwa klabuni, akivuta kiasi cha pauni 250 000 kwa wiki.

Nani nae alimaliza msimu uliopita akiwa Sporting, lakini Man United walimlipa kiasi cha pauni 110 000 kwa wiki.

Kwa ujumla, wakali hao walijikusanyia pamoja kiasi cha pauni 625 000 kwa wiki, zaidi ya jumla ya mshahara wanaopata nyota wapya waliosajiliwa msimu huambao ni kina Depay, Schwensteiger, Schneiderlin, na Darmian.

Schwensteiger ameripotiwa kuvuta kiasi cha pauni 220 000 kwa wiki, Schneiderlin na Depay pauni 150 000 kwa wiki kila mmoja, na Darmian analipwa pauni 100 000.

Ukijumlisha kwa pamoja wanakusanya pauni 620 000 kwa wiki ambayo imepungua kidogo ukilinganisha na nyota walioondoka.

Kocha Louis Van Gaal kwa sasa ndiye ametumia pesa nyingi zaidi katika dirisha la usajili, kiasi ambacho kinafikia pauni mil. 76.7 tayari kimetumika.
Mishahara ya nyota wapya waliosajiliwa Man United hii hapa. Mishahara ya nyota wapya waliosajiliwa Man United hii hapa. Reviewed by Steve on Saturday, July 18, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.