Propellerads

Hiki ndicho Pedro kawaambia watu wa karibu kuhusu Man United




Forward wa Barcelona, Pedro amedaiwa kuwaambia marafiki zake na familia kua
anatarajia kuelekea Manchester United majira haya ya joto.

Nyota huyo mwenye miaka 28 amekua hayumo katika kikosi cha kwanza tangu mwaka jana, ambapo ujio wa Luis Suarez ulimweka benchi.

Ripoti zinadai anataka kuondoka ili kupata timu atakayocheza kikosi cha kwanza, huku Man United nao wakitafuta nyota atakaye ziba nafasi ya Di Maria.

Telegraph wanadai kua tayari Pedro ameshafanya makubaliano na Man United kwa dau la £22m, lakini inasubiriwa Man United wamalize suala la Di Maria kwanza.

Hata hivyo Pedro mwenyewe anaonekana kuamini dili hilo litakamilika kwani tayari ameshaanza kuwaaga watu wake wa karibu.


Hiki ndicho Pedro kawaambia watu wa karibu kuhusu Man United Hiki ndicho Pedro kawaambia watu wa karibu kuhusu Man United Reviewed by Steve on Wednesday, July 29, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.