Propellerads

Gor Mahia sasa nusu fainali Kagame

Mahia ya Kenya imefanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano ya Kagame Cup baada ya kuitandika Malakia FC ya Sudan Kusini kwa goli 2-1 kwenye mchezo wa robo fainali uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa.



Godfrey Walusimbi amefunga magoli yote mawili ya Gor Mahia na kuivusha timu hiyo
hadi kwenye hatua ya nusu fainali. Ilichukua dakika mbili tu Gor Mahia kuandika goli la kwanza lililofungwa na mshambuliaji raia wa Uganda Godfrey Walusimbi kabla ya kufunga goli lingine dakika ya 27 kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili Malakia walionekana kucheza kwa nguvu na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara wakitafuta goli ambapo walifanikiwa kupata goli la kufutia machozi kupitia kwa Thomas Jacob Mathew. Kipindi cha pili Gor Mahia ilionekana kuridhika na matokeo ya kipindi cha kwanza kwa kucheza mpira wa taratibu huku wachezaji wake wakionekana hawahitaji tena kufunga goli.

Matokeo hayo ya leo yanazifanya Khartoum National Club na Gor Mahia kukutana kwenye mchezo wa nusu fainali, ikumbukwe timu hizi zilikutana kwenye hatua ya makundi zote zikiwa Kundi A na kutoka sare ya kufungana goli 1-1. Mchezo wao wa nusu fainali utakuwa ni wa pili kwenye mashindano haya ya Kagame mwaka huu.

Kesho pia itapigwa michezo miwili ya robo fainali , mchezo wa kwanza utakuwa saa 7:45 mchana kati ya KCCA ya Uganda dhidi ya Al Shandy ya Sudan wakati mchezo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wengi wa soka ni ule wa Azam FC dhidi ya Yanga mchezo utakaopigwa majira ya saa 10:00 jioni michezo yote ikipigwa kwenye uwanja wa Taifa.

Michezo ya nusu fainali itapigwa siku ya Ijumaa wakati mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu pamoja na mechi ya fainali itachezwa siku ya Jumapili.
Gor Mahia sasa nusu fainali Kagame Gor Mahia sasa nusu fainali Kagame Reviewed by Steve on Wednesday, July 29, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.