Bartomeu ashinda tena uraisi Barca
Josep Maria Bartomeu amechaguliwa tena kuwa raisi wa Barcelona kwa
muhula wa pili, akimshinda Joan Laporta ambaye ameshawahi kuwa raisi wa klabu hiyo.
Taarifa kutoka kituo cha habari cha Barcelona kinasema kwamba Bartomeu alipata kura asilimia 54.63 ambazo zilipigwa jana Jumamosi.
Bartomeu kwa ushindi huo ina maana ataiongoza klabu ya Barcelona kwa miaka sita mingine.
Bartomeu alipata kiti cha uraisi baada ya raisi aliyekuwa mwanzo Sandro Rosell kujiuzulu kufuatia shutuma zilizokuwa zinamkabili juu ya usajili wa Neymar kutoka Santos.
Bartomeu akiwa amefanikia kuisimamia Barcelona kupata ubingwa wa Copa del Rey, La Liga na Klabu Bingwa Ulaya aliweza kumshinda mpinzani wake Joan Laporta ambaye aliongoza klabu hiyo kuanzia 2003 mpaka 2010
Bartomeu ashinda tena uraisi Barca
Reviewed by Steve
on
Sunday, July 19, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, July 19, 2015
Rating:
