Propellerads

Nyota wa Simba aenda mazoezi ya Yanga.




Mambo yanakwenda yanabadilika, sasa si kama zamani! Zikiwa zimepita siku mbili tu tangu kuonja mazoezi na timu yake mpya ya Simba, kiungo wa timu hiyo, Peter Mwalyanzi, juzi Jumatano aliivamia Yanga kwenye mazoezi.

Kiungo huyo aliyetokea Mbeya City, aliifuata Yanga wakati timu hiyo ikiwa katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Friends Rangers kwenye Uwanja wa Karume, mchezo ambao ulichukuliwa kama mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao.

Simba na Yanga ni timu pinzani zaidi Tanzania na mara nyingi wachezaji wake wamekuwa wagumu kuchanganyika pamoja katika ishu mbalimbali zinazohusiana na mambo ya soka.

Mwalyanzi alifika mazoezini hapo kwa lengo la kumuangalia ‘mshkaji’ wake Deus Kaseke ambaye walikuwa wakikipiga pamoja Mbeya City msimu uliopita lakini kwa sasa ni mali ya Yanga.

Mwalyanzi alipoulizwa sababu za kufika uwanjani hapo alicheka tu na kutotaka kufafanua zaidi.


Mbali na Mwalyanzi, pia kulikuwa na wadau mbalimbali wa Simba katika mchezo huo, akiwemo makamu wa rais wa timu hiyo, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ pamoja na kinda wa timu hiyo, Issa Abdallah.
Nyota wa Simba aenda mazoezi ya Yanga. Nyota wa Simba aenda  mazoezi ya Yanga. Reviewed by Steve on Friday, June 26, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.