Mgogoro wa Manji na Mengi.....hatimae mdahalo kufanyika Ijumaa hii.
Mdahalo unaosubiriwa kwa hamu kubwa kati ya Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji dhidi ya Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi sasa utarushwa moja kwa moja na runinga ya ya Taifa ya TBC. |
Kwa mujibu wa mtandao wa www.manjivsmengi.com, mdahalo huo wa utarushwa Ijumaa Juni 3 kuanzia Saa 12 jioni hadi saa 1 usiku.
Mdahalo huo umeandaliwa na Manji ambaye amemualika Mengi na kutaka atoe uthibitisho kuwa kweli yeye ni fisadi.
| Manji amesema iwapo itabainika kweli yeye ni fisadi na wananchi kupiga kura kupitia ujumbe mfupi kutokana na kile kitakachozungumzwa kwenye mdahalo, basi ataachia ngasi uenyekiti wa Yanga. |
Manji amesisitiza yuko tayari kuachia ngazi kwa kuwa Yanga inapaswa kuongozwa na watu wa wasafi.
Amesema yeye ni mtu msafi, lakini amekuwa akiumizwa kutokana na kushambuliwa na vyombo vya habari vya IPP bila sababu za msingi.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari, wiki iliyopita, Manji alisisitiza kama Mengi atashindwa kwenye mdahalo, basi aiache Yanga iendelee na utulivu kuliko kutaka kuivuruga kwa makusudi.
Mgogoro wa Manji na Mengi.....hatimae mdahalo kufanyika Ijumaa hii.
Reviewed by Steve
on
Tuesday, June 30, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Tuesday, June 30, 2015
Rating:

