Mambo matano usiyoyajua kuhusu Firmino wa Liverpool.
Forward Mbrazil Roberto Firmino amesajiliwa na Liverpool kwa dau la pauni mil. 29 akitokea
Hoffenheim ya Ujerumani, na leo nakuletea mambo matano ambayo inawezekana ukawa hauyafahamu.
1) Mbrazil huyu anatokea katika mji wa Maceio huko Brazil, mji huu pia ndipo anapotokea mshindi mara tatu wa kombe la dunia , Mario Zagallo, ambaye alichukua kombe hilo mara mbili kama mchezaji na mara moja kama kocha.
2) Akiwa na umri wa miaka 14 pekee, Firmino alihamia mji wa Frolianopolis ambao upo umbali wa km 3 000 kutoka ilipo familia yake, alienda huku kujaribu bahati yake katika soka. Ulipita mwaka mzima bila ya kuonana na mama yake , lakini hii haikumzuia yeye kutimiza ndoto zake.
3) Alianza kucheza kama mchezaji Professional mwaka 2009 na timu ya Figueirense ambayo ilikua Serie B Brazil. Alifanikiwa kucheza michezo 38, akifunga magoli 8, kabla hajajiunga na Hoffenheim ya Ujerumani mwaka 2011.
4) Nyota huyu anamhusudu sana Ronaldinho kama mtu aliyemvutia, lakini hata hivyo anawazimia nyota wengine kama Ronaldo, Romario na Rivaldo.
5) Firmino alianza kucheza kuonekana na timu ya taifa ya Brazil Novemba 12, 2014 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Uturuki, na siku sita baadaye akafunga goli lake la kwanza katika timu ya taifa.
Mambo matano usiyoyajua kuhusu Firmino wa Liverpool.
Reviewed by Steve
on
Thursday, June 25, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Thursday, June 25, 2015
Rating:
