Gerard afichua mechi iliyomfanya aondoke Liverpool.
Mkongwe wa klabu ya Liverpool, Steven Gerard amefichua wazi mechi iliyomfanya aamue kuondoka
klabuni hapo, ameyasema hayo wakati wa interview na mkongwe mwingine wa Man United, Rio Ferdinand.
Nahodha huyo wa zamani wa Liverpool alikua akizungumza na Rio Ferdinand kuhusu mambo mbali mbali juu ya soka lake Liverpool, pia kuondoka kwake kwenda La Galaxy.
Liverpool walipata kukutana mara mbili na Real Madrid msimu uliopita katika michuano ya klabu bingwa, ambapo Gerard alikaa benchi, na ndio kitu kilichomfanya aamue kuondoka.
"Vizuri, unanijua mimi" alimwambia Rio Ferdinand kwa mujibu wa Daily mail
"Hii ilitokea katika kipindi ambacho nilikua nawaza nini kitafuata kwangu, na nilikua nimeshafanya mazungumzo mara kadhaa na Brendan akasema ataanza kunipangia michezo yangu-'nataka nianze kukuangaliana nataka uwe vizuri, sitaki ucheze michezo mitatu kwa wiki, kwani utachoka'-ndivyo alivyoniambia.
"Nilipoambiwa, sikua nacheza tena kwa ajili ya timu, bali kwa ajili ya mahusiano yangu na Brendan, nilichukulia hivyo na nikakubali.
"Lakini nilipokaa benchi nilichanganyikiwa, nilitaka kucheza.
"Ilinisukuma mimi kuchukua maamuzi ya kuondoka na kujaribu kufanya kitu kingine tofauti"
Baada ya maamuzi hayo, Gerard aliondoka, lakini anasisitiza kua mahusiano yake na kocha Brendan Rodgers yalikua mazuri.
Gerard amepata kucheza mara 689 akiwa na Liverpool na kufunga magoli 180, huku akitoa usaidizi zaidi ya mara 101.
Gerard afichua mechi iliyomfanya aondoke Liverpool.
Reviewed by Steve
on
Wednesday, June 24, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, June 24, 2015
Rating:
