Di Maria haondoki Man United, lakini adai hana furaha.
Nyota wa Man United, Angel Di Maria amedai hana furaha klabuni kwake, lakini amesisitiza
hataondoka msimu huu.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina alikua na wakati mgumu katika kua katika kiwango chake msimu uliopita alipojiunga Old Traford akitokea Real Madrid.
Katika kipindi hiki cha usajili zilienea tetesi ku Di Maria anataka kuondoka Man U ,huku Paris Saint Germain ikitajwa sana kutaka kumnasa, lakini hata hivyo mwenyewe amesisitiza hawezi kuondoka kwa sasa.
Di Maria aliulizwa katika interview na gazeti la Ole kama ana mpango wa kuondoka ambapo alijibu
"Hapana, kwa sababu sifikirii hivyo. Hata Real Madrid kuna wakati nilikua napata wakati mgumu uwanjani, lakini nilikabiliana na hiyo hali na kisha kuendelea. Napenda kupambana na mambo"
Pamoja na kuendelea kukaa, lakini amedai kua hana furaha kutokana na kukosa nafasi ya kutosha kucheza, ambapo aliongeza "Ndio, kwa ajili yangu na familia yangu, mambo hayaendi kama nilivyopanga, kwa sababu sichezi"
"Kwa sababu nilikuja na malengo lakini nimeishia bench, ni ngumu kuelezea jinsi ninavyohisi nilianza vizuri kwa magoli na assists, nilikua na wakati mzuri, ni ngumu kuelezea kwa nini sichezi"
Huko nchini Hispania iliripotiwa kua Barcelona walifanya mazungumzo na Di Maria, ikitarajiwa kua huenda baadae akahamia klabuni Nou Camp.
Di Maria haondoki Man United, lakini adai hana furaha.
Reviewed by Steve
on
Thursday, June 25, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Thursday, June 25, 2015
Rating:
