Hatimaye Adebayor apewa muda wa kupumzika.
![]() |
| Emmanuel Adebayor |
Mchezajii wa kilabu ya Tottenham Emmanuel Adebayor amepewa mapumziko kwa
mara ya pili msimu huu lakini hatma yake
katika kilabu ya Spurs
haijulikani.
Mchezaji huyo wa taifa la Togo mwenye umri wa miaka 31 ameandika
kuhusu matatizo ya famili yake katika mtandao wa facebook na kusema kuwa
alikuwa ameamua kujiuua.
Atakosa mechi ya siku ya jumapili kati ya kilabu yake na Everton mbali na ziara ya Kuala Lumpur na baadaye nchini Sidney.
''Tumempa
mda wa kusuluhisha mzozo na familia yake'',alisema kocha wa kilabu hiyo
Mauricio Pochettino.Ni miasha yakje ya kibinafsi .Niliongea naye mapema
wiki hii,ni hali ngumu kwake''.
Adebayor alijiunga na klabu ya
Spurs mwaka 2011 kutoka Manchester City kupitia mkopo kabla ya mabao 18
aliyofunga akiwa na Hotspurs kumwezesha kupewa kandarasi ya kudumu.
Hatimaye Adebayor apewa muda wa kupumzika.
Reviewed by Steve
on
Sunday, May 24, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, May 24, 2015
Rating:
