Propellerads

Wakati Simba wakimuwinda Ngoma, Yanga nao wampimia Ajibu, mipango ipo namna hii




Wakati Ligi kuu Tanzania bara inaelekea ukingoni, vita ya usajili kwa
mahasimu wa soka nchini imeanza chini chini, huku Yanga ikitajwa kupania kumchukua mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajib kwa udi na uvumba.

Mmoja kati ya wadau waandamizi wa Yanga aliyepata kushika nafasi ya uongozi katika klabu hiyo amefunguka kwamba Ajib atavaa jezi za Yanga msimu ujao.

Alisema walishazungumza naye kwa kirefu mshambuliaji huyo na kilichopo wanasubiri amalize mkataba wake na Simba Juni mwaka huu ili taratibu nyingine za kutua Yanga zifanyiwe kazi.

Ajibu aliingia kwenye mgogoro wa kimkataba na klabu yake ya Simba mwezi Disemba mwaka jana akidai mkataba wake umechezewa, kwani ulipaswa kumalizika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu Tanzania Bara mwaka jana.

Hata hivyo baada ya mvutano na uongozi wa Simba ambao ulidai kuwa bado ana mkataba na klabu hiyo wa miezi sita na kumshawishi kuongeza mkataba, lakini aligoma.

"Inaoneka wenzetu (Simba) wanatumia nguvu kubwa kutaka kumchukua Ngoma (Donald), basi na sisi hili la Ajib tumeamua tulifufue, wao wamchukue Ngoma, sisi Ajib.

"Ndiyo soka la Bongo lilivyo wewe ukifanya hivi wenzio wanafanya vile," alisema kiongozi huyo kwa kujiamini, huku akiomba asitajwe jina kwa vile wenzake hawataki lijulikane kwa sasa.

Ajibu mwenyewe alipoulizwa kuhusu swala hilo, alitoa majibu haya "Mpira kwangu ni kazi, mwenye kisu kikali ndiye anakula nyama, timu yenye maslahi mazuri ndiyo nitakayosajili, kwa sasa siwezi kuzungumza chochote kuhusu mkataba wangu.

"Siwezi kusema nabaki Simba au naenda Yanga, ligi ikiisha nitatuliza akili kabla ya kuamua naenda timu gani, kwa sasa tuyaache hayo," alisema Ajib.
Wakati Simba wakimuwinda Ngoma, Yanga nao wampimia Ajibu, mipango ipo namna hii Wakati Simba wakimuwinda Ngoma, Yanga nao wampimia Ajibu, mipango ipo namna hii Reviewed by Steve on Sunday, March 12, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.