Propellerads

Hivi ndivyo Simba wamewanyoa Polisi Dodoma kwa mabao matatu jana



Simba imeendelea na kasi yake ya kuonyesha ubabe, baada ya jana
kuitandika bila huruma timu ya Polisi Dodoma kwa jumla ya mabao 3-0 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Simba ilitakata katika mchezo huo kupitia kwa nyota wake, Shiza Kichuya, Laudit Mavugo na Juma Luizio.

Kichuya ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzitikisa nyavu za Polisi kwa bao safi kabla Mavugo kutupia la pili huku Luizio akifunga la tatu.

Simba imeendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya kusaka ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa sasa inaongoza kwenye msimamo ikiwa na jumla ya pointi 55.

Kikosi hicho kilitua Dodoma baada ya kupata mwaliko na kimejipanga kushiriki mechi mbalimbali za kirafiki wakati huu wa mapumziko ya ligi kuu kabla ya kurejea kuendelea kuwania ubingwa huo.
Hivi ndivyo Simba wamewanyoa Polisi Dodoma kwa mabao matatu jana Hivi ndivyo Simba wamewanyoa Polisi Dodoma kwa mabao matatu jana Reviewed by Steve on Sunday, March 12, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.