Propellerads

Haya ndio mambo matatu ambayo Simba wamewapiga bao wapinzani wao Yanga kwa msimu huu



Simba imethibitisha kuwa ni bora baada ya kuwazidi wapinzani wao
wa jadi, Yanga mambo matatu muhimu kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Mambo hayo matatu ambayo Simba wamewazidi Yanga ni kwamba, kwanza ndio wanaoongoza ligi wakiwa na pointi 55, pili ndiyo timu pekee yenye ukuta wa chuma kutokana na kufungwa mabao machache kuliko timu nyingine na tatu imetoa wachezaji bora wa mwezi mara mbili.

Katika hilo la ukuta wake kuwa wa chuma ni kwamba, wamefungwa mabao 10 tu tofauti na timu nyingine yoyote huku Yanga wakifuatia kwa kuruhusu mabao 11, hivyo ikimaanisha kuwa Simba wapo juu kwenye safu ya ulinzi.

Kwa upande wa wachezaji waliotwaa tuzo ni Shiza Kichuya (Septemba) pamoja na Method Mwanjali (Desemba) huku Yanga wao wakijivunia Simon Msuva aliyetwaa tuzo hiyo Oktoba mwaka jana.

Kikubwa ambacho Yanga wamewazidi  Simba ni safu yao ya ushambuliaji kupachika mabao mengi kwani mpaka sasa wanayo mabao 49, huku Wekundu hao wa Msimbazi wakiwa na mabao 40. Simba wako mkoani Dodoma ambapo jana walicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Polisi Dodoma, ikiwa ni maandalizi ya kwenda Arusha kukipiga na timu ya Madini FC ya mkoani humo kombe la FA.
Haya ndio mambo matatu ambayo Simba wamewapiga bao wapinzani wao Yanga kwa msimu huu Haya ndio mambo matatu ambayo Simba wamewapiga bao wapinzani wao Yanga kwa msimu huu Reviewed by Steve on Sunday, March 12, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.