Baada ya kukosolewa sana, Wenger aja na majibu haya....azungumzia ni lini ataondoka na mipango ya sasa pia
Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesisitiza
kwamba hana hofu yoyote kuhusu hatima yake klabuni hapo lakini pia amefunguka kwamba bado hajajua kama ataendelea baada ya msimu huu kumalizika.
Mashabiki wengi wa Arsenal sehemu mbalimbali ulimwenguni wamekuwa wakipaza sauti kwamba Wenger aondoke akimaliza mkataba wake majira ya joto.
Pamoja na kupata upinzani huo kila kona, kikosi cha Arsenal jana kiliibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Lincoln City katika kombe la FA, ushindi huu unafatia kipigo kizito kutoka kwa Bayern Munich wa jumla ya mabao 10-2 katika michuano ya klabu bingwa Ulaya.
"Kwa sasa tumewavunja sana moyo mashabiki wetu. Tunataka kwenda Wembley na kushinda tena. Karibuni hatujakua katika hali nzuri klabu bingwa. Baada ya hapo tunahitaji kuwa sawa na tunahitaji wachezaji wawe vizuri kiakili," Wenger aliiambia BT Sport.
"Tusizungumzie sana kuhusu mimi kwa sababu mengi yametokea hivi karibuni. Katika maisha yangu nishadhihirisha kwamba ninatakiwa kuihudumia klabu hii kwa moyo wote na nitafanya hivyo kwa kipindi chote nitakapokuwa hapa. Mpaka lini? Sijajua mpaka wakati gani. Nimeonesha uaminifu mkubwa na napendelea zaidi hapa.
"Nazingatia zaidi katika kazi yangu na siku zote nafanya hivyo. Nawaacha watu wengine wajadili kiwango changu. Siku zote nafanya hivyo, sina hofu na mambo mengine ninajitahidi kufikiria mchezo unaofuata."
Baada ya kukosolewa sana, Wenger aja na majibu haya....azungumzia ni lini ataondoka na mipango ya sasa pia
Reviewed by Steve
on
Sunday, March 12, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment