Lwandamina afichua lilipo tatizo kwenye kikosi cha Yanga ila maamuzi yake yanategemea hivi....
Kocha wa Yanga, George Lwandamina amesema kinachosababisha
timu hiyo kutofanya vizuri ni baadhi ya wachezaji kushindwa kujitoa kuipigania timu yao kwenye baadhi ya mechi hasa za ligi.
Yanga inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi na hivi karibuni timu hiyo ilipoteza mchezo dhidi ya mahasimu wao Simba wliokuwa pungufu uwanjani.
Lwandamina amesema kama wachezaji wataamua kucheza kwa kujitoa na kuipigani timu yao, hakuna timu ambayo inaweza kuwafunga, lakini baadhi ya nyota hao wamekuwa wakicheza kwa kiwango ambacho, pindi wanapoamua jambo ambalo linamsononesha yeye na mashabiki wa timu hiyo.
"Hivi ni vitu ambavyo nimevikuta, ukizingatia mimi nimekuja katikati ya msimu na siwezi kuvibadilisha, lazima niendelee navyo, hadi pale msimu utakapokwisha ndipo nipandikize falsafa zangu, lakini hiki ninachokiona siyo rahisi kwa timu kubwa kama hii kufanikiwa," alisema Lwandamina.
Kocha huyo raia wa Zambia, alisema mipango yake ni kukifumua kikosi hicho na kukisuka upya kwa ajili ya msimu ujao na anaamini kitakuwa na mafanikio makubwa kutokana na malengo aliyokuwa nayo.
Lwandamina afichua lilipo tatizo kwenye kikosi cha Yanga ila maamuzi yake yanategemea hivi....
Reviewed by Steve
on
Sunday, March 12, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment