Zabaleta kuelekea West Ham, Uongozi wampa uamuzi Wenger...yote katika tetesi za Usajili magazetini Ulaya leo, cheki hapa
West Ham wapo katika mipango ya kumsajili beki wa Manchester City,
Pablo Zabaleta kwa mujibu wa gazeti la Uingereza la Mail on Sunday.
Beki huyo Muarjentina huenda akaangalia mlango wa kutokea Etihad majira ya joto, hii itategemea kama kocha Pep Guardiola bado hatompa nafasi ya kutosha ya kucheza.
West Ham wanaamini watafanikiwa kumnasa Zabaleta ikizingatiwa mkataba wake unamalizika mwezi June.
Lakini pia kuna tetesi huko kwingineko ambazo zimebamba katika magazeti ya Ulaya Jumapili hii;_
Arsene Wenger ameambiwa na bodi ya watendaji Arsenal kuwa kipindi cha mapumziko ya ligi kwa ajili ya michezo ya kimataifa anatakiwa kufanya maamuzi kuhusu hatma yake klabuni.
Jurgen Klopp ana mipango ya kufanya usajili wa nguvu kipindi cha majira ya joto.
Klabu ya Real Madrid wamempa muda mpaka kufikia mwezi May kuhusu maamuzi ya kurejea Hispania mlinda mlango wa Manchester United, David De Gea.
Jesse Lingard anajiandaa kufanya mazungumzo ya mkataba mpya klabuni Manchester United huku Tottenham Hotspurs wakimfatilia kwa karibu.
Hatima ya kocha wa Birmingham, Gianfranco Zola ipo katika hatihati baada ya wamiliki wa klabu kuhitaji mabadiliko.
Chelsea na Manchester City wapo katika mbio za kumnasa kuingo wa Sevilla, Steven N'Zonzi.
Chelsea na Arsenal wapo mcho 'kodo' kuhusu mkataba wa Jesse Lingard na klabu yake ya sasa Manchester United.
Chelsea wametakiwa kulipa kiasi cha pauni mil 30 kumsajili Ben Gibson kutoka Middlesbrough.
Zabaleta kuelekea West Ham, Uongozi wampa uamuzi Wenger...yote katika tetesi za Usajili magazetini Ulaya leo, cheki hapa
Reviewed by Steve
on
Sunday, March 12, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment