Propellerads

Kukosekana kwa Mwanjali, benchi la ufundi la Simba limesuka mipango hii spesho kuivaa Madini FC




Kukosekana kwa beki tegemeo wa Simba, Method Mwanjali,
kumelifanya benchi la ufundi la timu hiyo likiongozwa na kocha Joseph Omog kumpika upya beki wao, Juuko Murshid, ili ashirikiane vema na Abdi Banda itakapovaana na Madini FC.

Simba itavaana na Madini katika mchezo wa robo fainali wa michuano ya kombe la FA utakaopigwa Machi 18, uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.

Simba ilifanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo baada ya kuichapa African Lyon bao 1-0 katika hatua ya 16 bora.

Kurejea kundini kwa Juuko kunaifanya safu ya ulinzi ya timu hiyo kuzidi kuimarika, baada ya kutokuwapo kwa Mwanjali, ambaye aliumia wakati wa mchezo dhidi ya African Lyon.
Kukosekana kwa Mwanjali, benchi la ufundi la Simba limesuka mipango hii spesho kuivaa Madini FC Kukosekana kwa Mwanjali, benchi la ufundi la Simba limesuka mipango hii spesho kuivaa Madini FC Reviewed by Steve on Saturday, March 11, 2017 Rating: 5

1 comment:

this.mrisho said...

Nakumbuka Mwanjali aliumia mechi ya Tanzania Prisons.

Propellerads
Powered by Blogger.