Kukosekana kwa Mwanjali, benchi la ufundi la Simba limesuka mipango hii spesho kuivaa Madini FC
Kukosekana kwa beki tegemeo wa Simba, Method Mwanjali,
kumelifanya benchi la ufundi la timu hiyo likiongozwa na kocha Joseph Omog kumpika upya beki wao, Juuko Murshid, ili ashirikiane vema na Abdi Banda itakapovaana na Madini FC.
Simba itavaana na Madini katika mchezo wa robo fainali wa michuano ya kombe la FA utakaopigwa Machi 18, uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
Simba ilifanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo baada ya kuichapa African Lyon bao 1-0 katika hatua ya 16 bora.
Kurejea kundini kwa Juuko kunaifanya safu ya ulinzi ya timu hiyo kuzidi kuimarika, baada ya kutokuwapo kwa Mwanjali, ambaye aliumia wakati wa mchezo dhidi ya African Lyon.
Kukosekana kwa Mwanjali, benchi la ufundi la Simba limesuka mipango hii spesho kuivaa Madini FC
Reviewed by Steve
on
Saturday, March 11, 2017
Rating:
1 comment:
Nakumbuka Mwanjali aliumia mechi ya Tanzania Prisons.
Post a Comment