Propellerads

Mkude asisitiza dhamira ya Simba ni moja tu....



Nahodha wa klabu ya Wanamsimbazi Simba, Jonas Mkude
amesema wamepanga kuhakikisha wanashinda mechi zote zilizobaki ili waweze kutwaa ubingwa ligi kuu msimu huu.

Simba sasa hivi ipo kileleni ikiwa na pointi 55 na nyuma yake wapo Yanga wenye alama 53 na wote  wamecheza mechi 24. Simba wanahaha kuhakikisha wanatwaa ubingwa huo ambao mara ya mwisho kuutwaa ilikuwa na msimu wa 2011/12.

Mkude alisema kuwa, wamejipanga kuhakikisha wanajituma kwa nguvu zote uwanjani ili wafanikiwe kupata ushindi katika michezo yote sita iliyobaki.

"Tunahitaji kushinda mechi zote zilizobakia ili kuweza kutimiza lengo letu kwani dhamira yetu ni ileile ya kutwaa ubingwa msimu huu, hivyo tunahitaji kuungana katika kipindi hiki cha mwisho kwa kuendelea kuimarisha umoja wetu kuanzia wachezaji, viongozi na mashabiki kwa ujumla," alisema Mkude.
Mkude asisitiza dhamira ya Simba ni moja tu.... Mkude asisitiza dhamira ya Simba ni moja tu.... Reviewed by Steve on Saturday, March 11, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.