Propellerads

Wenger sasa amepata kiburi, ona ujumbe aliotuma kwa mahasimu wake




Arsene Wenger amedai kwamba ushindi wa Arsenal dhidi ya Hull City
wikiendi hii umethibitisha kwamba kikosi chake kipo tayari kuleta changamoto katika kuchukua ubingwa wa EPL.

Gunners walicheza mchezo wa kuvutia ugenini kwa kuwafunga wapinzani wao mabao 4-1 Jumamosi jioni.

Wenger amefurahishwa jinsi Arsenal walivyoweza kuutawala mchezo na akidai ujumbe umeshatumwa kwa vilabu pinzani kwao.

"Hili ni tangazo la ushindi," alisema kama alivyonukuliwa na The Telegraph "Tulifunga matatu kwa Watford, tumefunga manne dhidi ya Hull. Tulipata 0-0 kwa Leicester, lakini tulikua na nafasi mbili au tatu. Ugenini tumeweza kuwa na nafasi kuliko nyumbani.

"Naamini kwamba tulipopoteza mchezo wetu wa kwanza ulikua ni mshtuko kwetu na mashabiki wetu. Mara moja unakua na wasi wasi na mashaka, Kwa hiyo ilikua ni muhimu kwetu kushinda mchezo wa Southampton na ninaamini sasa tunaweza kuwa na ubora huo huo nyumbani."
Wenger sasa amepata kiburi, ona ujumbe aliotuma kwa mahasimu wake Wenger sasa amepata kiburi, ona ujumbe aliotuma kwa mahasimu wake Reviewed by Steve on Monday, September 19, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.