Mourinho amejitetea kwa kumchezesha Martial akiwa ameumia
Kocha Jose Mourinho amejitetea kwamba hakuwa
anafahamu chochote baada ya kumchezesha Anthony Martial ambaye ana majeraha kichwani baada ya kupata mitikisiko.
Martial alikaa uwanjani kwa karibia dakika 10 pamoja na kupewa matibabu baada ya kugongana kichwa na Daryl Janmaat, lakini hata hivyo alitoka nje dakika ya 34.
Mourinho amedai kwamba hakua na uhakika na kiasi Martial alivyoumia "Sijui, ninakiri sifahamu. Mnauliza vitu ambavyo siweze kuwaambia. Nilitakiwa kuwa mchezoni muda ule na sio kuwa na shaka kuhusu Anthony.
"Haikuniwi ugumu kuangalia hali ile. Hakikua kitendo cha kwenda hospitali.
"Sikujua kwanini alitoka, kwamba ameumia goti lake, kiwiko, au kichwa. Sijui. Sijui kwamba hakua kwenye hali nzuri kuendelea. Sijajua kilichotokea."
Mourinho amejitetea kwa kumchezesha Martial akiwa ameumia
Reviewed by Steve
on
Monday, September 19, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment