Kufuatia kufungwa kwa mara nyingine tena Mourinho amegundua ugonjwa unaosumbua kikosi chake
Bosi wa Manchester United, Jose Mourinho amefunguka kwamba
kinachowahangaisha wachezaji wake kwa sasa ni hofu inayotokana na kufungwa mfululizo.
Red Devils wamepigwa kwa 3-1 na Watford katika mchezo wa Premier League leo hali iliyopelekea kocha huyo mreno kuwaza kuhusu saikolojia ya wachezaji wake.
Hot topic: Nini kinaigharimu Man United ya Mourinho msimu huu?!
"Tulianza msimu vizuri na tulikua na matokeo mazuri. Nadhani kwa mara ya kwanza tumeshindwa, tumekuwa na wakati mgumu, baadhi ya vijana wana wakati mgumu kuendana na hali ya kushindwa," aliiambia BBC Sport.
"Umeona Ashley Young kujiamini kwake na furaha alikoleta mchezoni ni kitu ambacho mchezaji anatakiwa kuwa nacho."
Kufuatia kufungwa kwa mara nyingine tena Mourinho amegundua ugonjwa unaosumbua kikosi chake
Reviewed by Steve
on
Sunday, September 18, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment