Ratiba ya Manchester Derby inampa hofu Mourinho kutokana na sababu kadhaa
Bosi wa Manchester United, Jose Mourinho ameoneshwa kupata walakini kutokana
na ratiba ya mechi ya kwanza Manchester Derby, imeripoti Manchester Evening News.
Red Deviks watawakaribisha Manchester City tarehe 10 Septemba, ikiwa ni mchezo wao wa kwanza baada ya mapumziko ya kimataifa.
Kiasi kikubwa cha wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Mourinho wameondoka kuchezea timu zao za taifa, huku Mourinho akidai kua wale wanaotoka Amerika ya kusini watarejea Carrington ikiwa yamesalia masaa 24 pekee kabla ya mchezo.
Hii ikiwa na maana kwamba Antonio Valencia, Marcos Rojo na Sergio Romero watakua na kipindi kimoja pekee cha mazoezi kabla ya mpambano na mahasimu wao.
Aliiambia MUTV "Tuna wachezaji nane hawapo na kipa Sam Johnstone.
"Tunapoteza wengine tena na hatujui namna gani wanafanya mazoezi, jinsi wanavyotibiwa, jinsi maisha yao yanavyoenda kua na timu zao za taifa.
"Baadhi watarejea Jumatatu kabla ya mechi ya Manchester City lakini wengine watarejea Ijumaa."
Ratiba ya Manchester Derby inampa hofu Mourinho kutokana na sababu kadhaa
Reviewed by Steve
on
Friday, September 02, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, September 02, 2016
Rating:




No comments:
Post a Comment