FA wanamtaka Wenger kuifundisha England, mwenyewe ameamua hivi
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amefunguka kwamba ameshangazwa
na tetesi zinazomhusisha yeye na kibarua cha kuifundisha timu ya taifa ya England.
Mfaransa huyo amekua akifukuziwa na FA kwa muda mrefu sasa, ambapo ripoti zikidai kwamba uongozi unaweka mipango sawa kuzungumza na kocha huyo kufuatia kuondoka kwa Sam Allardyce wiki iliyopita.
Akizungumza baada ya Gunners kupata ushindi klabu bingwa mbele ya Basel jana usiku, Wenger amefunguka kwamba kwake ni "surprise'.
"Ki ukweli, kwa sababu nililenga kwenye mchezo wa leo usiku. Sikufatilia sana, lakini ni suprise kubwa kwa kilichotokea." aliwaambia waandishi kwenye mkutano baada ya mechi.
Aliulizwa kuhusu stori zilizozagaa za yeye kutakiwa kuifundisha England alijibu "Bila shaka, lakini mara nyingi nimekua nikipendelea zaidi hii klabu mpaka mwisho wa msimu nitakua hapa. Nimelenga zaidi kwenye hili."
Mkataba wa sasa wa Wenger na Gunners unamalizika mwishoni mwa msimu huu na meneja huyo amefunguka kwamba hawezi kujihakikishia kwamba ataendelea kubaki Emirates.
"Hiyo haiamui", alisema "Nimeshasema mara nyingi napendelea zaidi klabu ya Arsenal na nitajitathmini mwenyewe kiasi gani nitakua nimefanya vizuri mpaka mwisho wa msimu huu."
FA wanamtaka Wenger kuifundisha England, mwenyewe ameamua hivi
Reviewed by Steve
on
Thursday, September 29, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment